Skip to main content

Posts

Showing posts from June 1, 2025

‘WIZARA YA KATIBA TANZANIA: ‘WANANCHI KOKOTA NENDENI SERIKALINI KUTAFUTA NYARAKA’

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WIZARA ya Katiba na Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imewataka wananchi wa Kisiwa cha Kokota shehia ya Mtambwe kusini wilaya ya Wete, kuendelea kuzitumia mamlaka za serikali, ili kupata ufumbuzi wa matatizo yao ya kisheria. Kauli hiyo imetolewa Juni 6, 2025 na Afisa Habari wa wizara hiyo, Pilly Nashon wakati akizungumza na wananchi hao, kwenye mkutano wa wazi, wa ufungaji wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria wa Mama Samia. Alisema, kwa wananchi hakuna namna ya kuzitumia mamlaka ya serikali kwa kutafuta haki zao, maana vyenginevyo wanaweza kupewa nyaraka, mfano wa vyeti vya kuzaliwa visivyohalali. Alieleza kuwa, nyaraka hizo pamoja na vyeti vya ndoa, hati za ardhi, vitambulisvyo ya taifa na vile vya ukaazi vya Zanzibar, vitaendelea kutolewa na mamlaka za serikali na wananchi wanapovihitaji waelekee huko. ‘’Jiepusheni na kuwatumia watu kwa umaarufu wao, mnapohitaji nyaraka mbali mbali, kama vile vitambulisho vya taifa na vyeti vy...

'FUATILIENI VYETI VYA KUZALIWA VYA WATOTO WENU NI HAKI KISHERIA'

  NA HAJI NASSOR PEMBA@@@@  WANANCHI wa shehia za Msuka mashariki, magharibi, Kifundi, Konde na Kinowe wilaya ya Micheweni, wamekumbushwa kufuatilia haki ya cheti cha kuzaliwa kwa  watoto wao, kwani kwa sasa ni jambo la lazima, kwa maisha ya sasa na baadae.   Ushauri huo umetolewa leo Juni 4, 2025 na Afisa Usajili wa Matukio ya kijamii wilayani humo, Alamas Massoud Hamad alipokuwa akizungumza na wananchi hao, kwenye mikutano ya muendelezo wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia.   Alisema hakuna namna kwa mzazi suala la kufuatilia cheti cha kuzaliwa kwa mtoto wake, kwani ni haki yake ya msingi kama ilivyo haki nyingine.   Alifahamisha kuwa, wajawazito wanapaswa kuhakikisha kwanza wanajifungulia hospitalini, ili iwe rahisi kuandikishwa na kukabidhiwa kipande chenye jina la mtoto husika.    Afisa huyo alieleza kuwa, uandikishwaji huo kisheria unapaswa kufanywa ndani ya siku 42 baada ya mtoto kuzaliwa na ikizidi hapo bado nafasi ip...

MICHEWENI WAKUMBUSHWA KUZISAJILI NDOA ZAO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KADHI wa wilaya ya Micheweni sheikh Mansab Khamis Omar, amewakumbusha waumini wa dini ya kiislam wa wilaya hiyo, kuzisajili ndoa zao, ili kupata cheti kinachotambulika.   Kadhi huyo, aliyasema hayo l eo Juni 3, 2025  kwa nyakati tofauti, wakati akizungumza na wananachi hao, kwenye muendelezo wa mikutano ya kampeni ya kitaifa ya msaada wa sheria ya Mama Samia, iliyofanyika Tumbe na Chimba.   Alisema, unaposajili ndoa, kisha unakabidhiwa cheti ambacho kinaweza kusaidia pindi ikitokezea siuntafahamu katika maisha ya ndoa hapo baadae.   Alieleza kuwa, cheti hicho pia husaidia kupatikana kwa uhakika wa maandishi, iwapo mmoja kati ya wanandoa hao amefariki.   ‘’Cheti cha ndoa ni muhimu mno, maana kinaweza kukusaidia hata, unapoomba vyeti vyingine mfano cheti cha kuzaliwa kwa watoto watakaopatikana,’’ aliwakumbusha.   Katika hatua nyingine, Kadhi huyo wa wilaya ya Micheweni, aliwataka wazazi na walezi kusimamia kwa karibu ndoa za w...

WANANCHI NJUGUNI, SIZINI, MTEMANI WASIFIA KAMPENI YA KITAIFA YA MAMA SAMIA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@   WANANCHI wa shehia za Mtemani, Njuguni, Sizini na Mtemani wilaya ya Micheweni, wamesifu ujio wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Suluhu Hassan, kwa kupata uwelewa wa mambo kadhaa ya kisheria.   Hayo yameyasema leo Juni 2, 2025  kwenye mikutano tofauti ya wazi, iliyofanyika skuli za Sizini na Wingwi, ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Suluh.   Juma Haji Juma wa Kilindini, alisema sasa amepata ufahamu wa njia za kufuata, ikiwa atabaini cheti chake au cha mtoto wake, kimekosewa herufi.   Nae Aisha Juma Makame wa shehia ya Mtemani, amesema kwa sasa amaelewa njia tano za kuimiliki ardhi, jambo ambalo hapo awali, hakuwa anafahamu.   ‘’Ilikuwa sielewi kuwa, hata ukivunja pori baada ya miaka kadhaa, kama hajatokea mwenyewe, ardhi hiyo unaweza kuimboa hati za matumizi,’’alieleza.   Kwa upande wake Asha Makame Haji, amesema alichofaidika yeye, ni kupata ufahamu ju...

WATAALAMU WA SHERIA: ‘CHIPS KUKU ZISIWE CHANZO CHA UDHALILISHAJI’'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA @@@@ WANAFUNZI wa vyuo, skuli za msingi na sekondari za wilaya ya Micheweni, wametakiwa kujiepusha na kupokea zawadi ovyo ovyo zikiwemo chips kuku, kwani huwa ni chanzo za kudhalilishwa na baadhi ya watu.   Hayo yameelezwa leo Juni 2, 2025 na maafisa sheria kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Jeshi la Polisi, Maafisa  ustawi na wanasheria wingine, kwenye kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Suluhu Hassaan  inayoendelea .   Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Micheweni Bizume Haji Zume, alisema wapo baadhi ya wadhalilishaji, huanza kuwapa zawadi watoto ikiwemo chakula cha chips na fedha, hivyo ni vyema wakajiepusha  navyo .   Alieleza kuwa, wapo wengi ambao wameshadhalilishwa kwa kuwa rahisi kupokea zawadi ambazo mwisho wake, hudhalilishwa na kufanyiwa ukatili.   ‘’Wanafunzi, mhakikishe hampendi kupokea zawadi za ovyo ovyo, kama chips na fedha na hata msaada wa usafiri ‘lift’ kwa watu wasiowafahamu,  m...

‘WANANCHI MICHEWENI ZIRASIMISHENI ARDHI ZENU’

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia za Majenzi, Chamboni, Micheweni, Shumba mjini na Mjini wingwi wilaya ya Micheweni Pemba, wamekumbushwa kuzirasimisha ardhi zao, mara baada ya kuzimiliki, ili kujiepusha na migogoro isiyokuwa ya lazima.   Ushauri huo umetolewa leo Juni 1, 2025  na Mkuu wa Idara ya Upimaji na Ramani Pemba, Salim Khamis Haji, alipokuwa akizungumza na wananchi hao, kwenye muendelezo wa kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkutano uliofanyika skuli ya Micheweni.   Alisema, migogoro kadhaa hujitokeza, kwa wananchi waliowengi kushindwa kuzirasimisha ardhi zao, katika taasisi husika, na kusababisha siuntafahamu baina ya pande moja na nyingine.   Alieleza kuwa, njia za kumiliki ardhi kisheria zipo tano ikiwemo kununua, kupewa na serikali, kuvunja pori, kurithi pamoja na kupewa zawadi ingawa kisha kinachofuata ni kuzirasimisha na kupata hati za matumizi.   ‘’Niwanasihi wananchi wenzangu wa wilaya ...

KAMPENI YA MAMA SAMIA YA KISHERIA YATANGAAZWA KWA WANAFUNZI MICHEWENI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@@ KAMPENI ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan, imetangaazwa kwa wanafunzi wa skuli ya skondari ya Maziwang’ombe na wale wa Chuo cha kiislamu Micheweni.   Wataalamu wa masuala ya kisheria kutoka ofisi za Mkurugenzi wa Mashtaka, Jeshi la Polisi, Mawakili wa kujitegemea, Maafisa ustawi wa jamii na wanasheria wa halmashauri, walifika leo Juni 1, 2025  kwenye kampeni maalum inayoendelea.   Wakizungumza kwenye mikutano hiyo ya wazi, walisema kampeni hiyo inakuja kuwaelezea wananchi na hasa wanawake, watu wenye ulemavu, waliomo kwenye makundi maalum na wasiokuwa na uwezo, kujua haki na wajibu wao kisheria.   Inspekta Saleh Ame Makame kutoka kituo cha Polisi Chake chake, aliwataka wanafunzi hao, kuripoti wanapoona viashiria vya udhalilishaji dhidi yao na wasivifumbie macho.   Alisema, kama lengo la kampeni hiyo ni kuwaelezea haki na wajibu wao, hivyo wahakikisha wanawaripoti wanao...