NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ “NIWEKEE kisongo pawa 2000, supu weka nyingi na pili pili kwa mbali na kiungwa”, lugha za kuagizia supu ya Mwata. Sio lugha ngeni kwa wafanya biashara na watu wanaouza supu hiyo ya Mwata hususan katika maeneo ya Kangani na vitongoji vyake. Wenyewe hutumia jina la “kisongopawa”kama umaarufu lakini jina halisi ni Mwata, ndilo watu wengi kutoka maeneo mbali mbali hufahamu kwa haraka. Na jina la kisongopawa si rasmi na si lenye kufahamika isipokua kwa wenyeji wa maeneo ya Kangani na jirani ambako ndio mwata huvuliwa na kuliwa . Mwata ni aina ya viumbe vipatikanavyo pwani, ambacho hutumiwa kwa ajili ya chakula au kitoweo kama ilivyo viumbe vingi vya baharini, ingawa umetofautiana navyo kwa kiasi kikubwa hata uvuvi wake. Mwata kisiwani Pemba hupatikana zaidi na kuhesabiwa kama ni kitoweo adhimu katika Pwani ya Jemele iliopo shehia ya Kangani wilaya ya Mkoani mkoa wa kusini Pemba. Ingawa baadhi ya watu hueleza yapo maeneo min...