NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@ MKURUGENZI Rasilimali watu utawala na mipango wa Tume ya Utangazaji Zanzibar ‘TUZ’ Zainab Sheha Khamis amesema, kushirikishwa kwa wadau mbali mbali katika kuchangia kanuni ya maudhui na udhibiti wa vituo vya utangazaji, kutasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa na tume hiyo. Aliyasema katika mkutano wa mafisa wa Jeshi la Polisi wa kitengo cha kupambana na uhalifu wa mtandaoni, kuhusu udhibiti wa maudhui kwa vituo vya utangazaji, kuelekea uchaguzi mkuu 2025 uliyofanyika ukumbi wa mikutano ZBC Mkoroshoni Chake Chake Pemba. Alieleza kuwa, kwa kushirikiana na wadau hao kutasaidia kufikia malengo husika, ya kupambana na uhalifu wa kimitandao, kuhusu maudhui kwa vituo vya utangazaji, ili kuepusha migogoro inayoweza kutokezea. "Tumeona wadau hawa ni muhimu, katika kushirikiana nao kwani wao ni sehemu moja wapo ya kuhakikisha wanadhibiti maudhui yaliyokua siyo na kupambana na uhalifu katika mitandao,"alifafanua. ...