ZANZIBAR Na Nafda Hindi, ZANZIBAR @@@@ WANANCHI wa Shehia ya Kigongoni Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja walalamikia umbali wa masafa marefu kwa watoto wao wakifuata huduma ya Elimu. wameiomba serikali kuwajengea skuli karibu na makaazi yao ili Watoto wao wapate elimu ipasavyo na kuwaepusha na hali hatarishi. Malalamiko hayo yamekuja kufuatia ziara ya kuibua changamoto za wananchi iliyoandaliwa na Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar kupitia mradi wa kuwainua wanawake katika Uongozi, Strengthen Women In Leadership (SWIL) unaotekelezwa na chama hicho. Wazazi wa watoto hao wamesema kwa sasa Watoto wanasoma skuli ya mbali ambayo wanatembea Zaidi ya saa moja hali inayohatarisha usalama wao na wengine kushindwa kufika skuli kuendelea na masoma na kuishia vichakani . “Skuli iko mbali na sisi inabidi twende Fukuchani. Kidagoni au Kidoti hali ambayo ina hatarish...