Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ABEDA ASAINI

KATIBU MKUU ABEDA ASAINI AGENDA YA MASUALA YA WANAWAKE KUHUSU AMANI, USALAMA

  NA MWANDISHI WETU, UNGUJA KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Abeida Rashid Abdallah amesaini Mpango wa Taifa wa kushughulikia Utekelezaji wa Agenda ya masuala ya Wanawake, kuhusu Amani na Usalama ulioandaliwa mahsusi kwa ajili ya kutekeleza Azimio Na:1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hafla ya utiaji saini imefanyika jana ofisini kwake Kinazini Unguja, amesema Mpango huo ni heshima kwa Tanzania kwani imeonesha wazi kukubali na kutekeleza Azimio hilo la Umoja wa Mataifa la kuhakikisha Wanawake wanakua  katika amani na usalama wakati wote. Amefahamisha kwamba Azimio hilo lilipitishwa tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka 2000, kwa lengo la kuhimiza umuhimu wa nafasi ya wanawake katika kuzuia na kutatua mizozo, mashauriano ya amani, ujenzi wa amani, ulinzi wa amani, hatua za usaidizi wa kibinadamu na ujenzi baada ya mizozo na kusisitiza umuhimu wa ushiriki sawa katika uendelezaji wa amani na usalama duniani. Ameeleza Wizara ya Maendeleo ya Jam...