NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAWAKE wa kijiji cha Mleteni shehia ya Kisiwani wilaya ya Wete, wameikumbusha serikali kuwajengea kituo chao cha Afya, kama ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, alivyoitoa wakati alipowatembelea. Walisema, tayari wameshakuwa na eneo ambalo walitakiwa kulitoa kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya, ingawa hadi sasa ni miezi zaidi ya mitano tokea Rais atowe ahadi, ingawa hakujaanza ujenzi. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, walisema wanahamu kubwa na kujengewa kituo hicho, ili sasa kwao iwe rahisi, kupata huduma mbali mbali zikiwemo za uzazi na mtoto. Walieleza kuwa, wamekuwa wakiifuata huduma hiyo eneo la Kisiwani ambapo pana umbali wa zaidi ya meli mbili, jambalo linalowapa ugumu, hasa kutokana na uchakavu wa barabara yao. Mmoja kati ya wanawake hao Aisha Nassir Sheha, alisema kutokana na umbali wa kituo cha afya hasa huduma za mama na mtoto, wengi wao wamekuwa hawa...