NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@ MJANE mwenye watoto saba amewaomba wahisani na watu wenye uwezo, kumpa msaada wa bati na miti, kwa ajili ya kuezekea nyumba yake, ili apate kustirika na watoto wake. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake kijiji cha Madenjani Wilaya ya Wete Pemba, leo Juni 12, 2025 mama huyo Rehema Salum, alisema nyumba anayokaa imeshakua mbovu, mvua yote inamnyeshea ndani mwake. Alisema anapatashida kwani mvua inaponyesha husimama barazani hata kama ni usiku mkubwa,kwa vile ndani hujaa maji na kukosa sehemu salama. ‘’Ndani hujaa maji, vitanda vyangu vyote vimeshaharibika sina hata pakulala na watoto wangu saba, naomba binadamu wezangu munisaidie nateseka,’’alilalamika. Alieleza tayari alishajenga vyumba viwili vya matufali, ingawa ameshindwa kuezeka, hivyo ameomba asaidiwe bati pamoja na miti kwa ajili ya kuezekea, ili apate kuishi sehemu anapostahiki binadamu. Alifahamisha kuwa mume wake amemuacha na watoto saba, na kumuachia mz...