NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR@@@@ MKURUGENZI Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee ndugu Hassan Ibrahim Suleiman amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Ustawi wa jamii unakuwa na wananchi wanaishi katika mazingira mazuri na salama. Akifungua mafunzo juu Sera ya hifadhi ya Jamii, yaliyofanyika katika ukumbi wa Sebleni,Unguja amesema ni vyema Idara hiyo kujenga mashirikiana na wadau mbalimbali kwani mtoto anahitaji kukua katika makuzi mema yatakayomjenga kuwa Raia bora kwa Taifa lake. “Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee inabeba jukumu zito hivyo, wanawajibu wa kushirikiana na kusaidia na wadau wengine katika kukuza ustawi wa jamii ili jamii waishi katika mazingira mazuri, hivyo nakuombeni mtowe mawazo yenu juu ya Sera hii, kwani maoni yenu yatasaidia kupata Sera bora” Alisema Hassan. Alieleza kwamba jamii inahitaji mambo mengi hasa ukizingatia kundi la kinamama wanaotelekezwa na watoto wao, wanakuwa ...