IMEANDIKWA NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@ MAAFISA Utumishi kwenye taasisi za Serikali na binafsi wametakiwa kutokuchelewesha mafaili ya watumishi wanaohitaji stahiki zao za mafao ZSSF, ili kuondosha usumbufu unaojitokeza wakati wa utekelezaji wa kazi hiyo. Akizungumza na maafisa hao katika Ukumbi wa kiwanja cha kufurahishia watoto Tibirinzi Chake Chake Pemba, Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (ZSSF) Pemba, Msabah Massoud Msabah alisema, kuna haja ya kuwa na Ofisa maalumu ambae atashughulikia mafaili hayo na sio kubadilishwa. Alisema kuwa, kumekuwa na ucheleweshwaji mkubwa wa mafaili ya watumishi ambao wanastahiki kupatiwa mafao yao kwa namna moja ama nyengine, jambo ambalo linaweza kuchukua muda mrefu kupatikana kwa haki, na wakati mwengene wanaweza kuikosesha kabisa, kwani kuna muda maalumu uliopangwa kwa ajili ya kuwasilisha vielelezo. “Tushirikiane pamoja katika hili kuhakikisha wanapatikana watendaji maalumu, ambao hata kwenye mafunzo watakuwa wanakuja hao hao kwa aj...