NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAZIRI wa Nchi, Ofis ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Mudrik Ramadhan Soroga, amesema miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar, imemletea heshima mzanzibari, kwa kupata haki zake bila ya ubaguzi, ikilinganishwa na kabla ya mwaka 1964. Alisema, kwa sasa kila mmoja anapata haki ya kuwasilisha lalamiko lake, katika vyombo vya sheria na kupokelewa kwa heshima na kisha kusikilizwa na uamuzi kutolewa kwa haki. Waziri Soraga, aliyasema hayo leo Disemba 22, 2023 mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la kituo cha Polisi cha wilaya ya Mkoani cha daraja ‘B’ ikiwa ni sehemu za shamra shamra za miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 1964. Alisema, sasa mzanzibari anatembea kifua mbele, akijua kuwa inapotokezea kubinywa kwa haki zake, anapopakukimbilia na kufungua mashauri, ambayo yanaendeshwa kwa haki kuanzia mwanzo hadi mwisho. Alieleza kuwa, waasisi wa taifa hili walipigania haki za wazalendo na mwendo huo unaendelezwa hadi leo ndani ya serikali ya Ma