NA TATU NAHODA, ZU@@@@ ……………fuata nyuki ule asali……………. Ndivyo walivyosema wahenga, wakimaanisha kuwa, unapaswa kufuata vitu, watu au sehemu zenye ujuzi, ili kufanikiwa katika malengo yako. Msemo huu unatumika katika nyanja nyingi ikiwemo ya wanafunzi wanaofuta elimu, hasa kwa mfumo wa kupitia maktaba ziwe na skulini au maeneo mingine. Maktaba ni hazina pekee inayomtajirisha mwenye kuhitaji utajiri wa kitaaluma na kimaarifa, kwani mtumiaji hapitwi na wakati, na hupata taarifa muhimu juu ya mambo mbali mbali. Kwa wanafunzi na walimu wao, maktaba imekuwa ni hazina yao ya thamani, kama alivyosema mtaalamu Marcus Tallus Cicore " if you have a garden and library you have everything you need " ukiwa na tafsiri isiyorasmi kuwa, kama una bustani na maktaba basi tayari una kila kitu. KWANINI MAKTABA NI MUHIMU SKULINI? Ahmed Khamis Ahmed mwanafunzi wa kidato cha pili skuli ya Madrasatul-Ahbaab Kisauni Unguja anasema, maktaba kwake ni suluhisho la ufumb