NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania ‘UWT’ taifa Mery Pius Chatanda, amesema aina ya Mbunge wa viti maalum mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, katika kuwakomboa wanawake kiuchumi, ndio mfano unaofaa kuigwa, na wabunge wengine Tanzania. Alisema, Mbunge huyo ameendelea kutekeleza kwa vitendo maagizo ya UWT taifa, ya kuwakomboa wanawake kiuchumi, kufuatia kukabidhi mashine ya kuzalisha mikate na tosi na fedha taslim, kwa wanawake wa mkoa wake, yenye thamani ya shilingi million 10.5 Mwenyekiti huyo wa UWT taifa, aliyasema hayo leo Oktoba 25, 2023, Micheweni mara baada ya kukabidhi mashine hiyo, kuweke jiwe la msingi ofisi ya ushoni wa nguo na kukabidhi shilingi milioni 1, zilizotolewa na Mbunge huyo. Alieleza kuwa, anaamini kupitia uwekezaji wa Mbunge huyo, wanawake wa CCM mkoa wa kaskazini Pemba, watapiga hatua kubwa ya kimaendeleo, kupitia njia ya kujiinua kiuchumi. Alifahamisha kuwa, wakati umefika kwa wabunge wengine wa mikoa ya Ta...