NA MWANDISHI MAALUM@@@@ MENEJA miradi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) Nairat Abdulla amewaomba wanawake kutumia vyombo vya habari kwa lengo la kutangaza kazi zao wanazozifanya. Akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wakulima viongozi kutoka shehia nne (4) za Unguja, juu ya umuhimu wa kutumia vyombo vya habari, yaliofanyika ofisi za TAMWA-ZNZ Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja, amesema wanawake wanajishughulisha na harakati mbalimbali zikiwemo za uzalishaji pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lakini bado sauti zao hazisikiki ipasavyo kupitia vyombo vya habari. Hivyo amewaomba wanawake hao kutumia vyombo vya habari hasa mitandao ya kijamii, kuelezea mafanikio na changamoto zinazowakabili katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili kufikisha ujumbe kwa wahusika na hatimae kupatiwa ufumbuzi. Akiwasilisha mada inayohusu vyombo vya habari, Meneja Mawasiliano kutoka TAMWA ZNZ, Sofia Ngalapi amesema wanawake waku...