Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Siti Abass Ali amesema Idara hiyo ipo katika mchakato wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbali kwa ajili ya kuifanyia maboresho sheria ya Mtoto namba sita (6) ya mwaka 2011 ili iendane na wakati uliyopo. Akizungumza katika kikao cha ukusanyaji wa maoni kilichowashirikisha wadau mbali mbali wakiwemo viongozi wa dini, wanasheria, Jeshi la Polisi, n.k katika ukumbi wa Skuli ya Kidonge Chekundu Unguja, jana alisema kutokana na vitendo vinavyojitokeza katika jamii,ikiwemo ajira za utotoni hivyo, idara hiyo imelazimika kuipitia sheria hiyo nakuja na maamuzi ya kuifanyia maboresha ili iendane na wakati . “Kwa kweli Sheria hiyo imetusaidia sana na inaenaendelea kutusaidia, imezungumza umuhimu wa mtoto kupata haki zake za msingi ikiwemo haki ya kupata elimu, matibabu, chakula, malazi, malezi, pia imezungumzia jinsi gani mtoto ataepukana na masauali ya udhalilishaji lakini baada ya kuipitia s...