NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ 'DUNIA imebadilika...kwani ya jana sio ya leo' Katika miaka ya sasa, wanaonekana wanawake wengi wanaojihusisha na masuala ya uongozi, katika sekta mbali mbali. Ikiwa ni katika vikundi vya ushirika, uongozi kwenye jamii, shehia, majimbo na hata kwenye taasisi za umma na binafsi. Hii ni kutokana na elimu inayotolewa kupitia vyombo vya habari na kwenye jamii, kuhusu ushirikishwaji wa wanawake kwenye masuala ya uongozi. Na ndio maana hata mfumo wa elimu uliopo sasa, unatambua kwamba watoto wa kike wanapaswa kujengwa mapema kiongozi, ili kila hatua anayopitia aweze kujiamini na kuwa jasiri. Tangu wakiwa skuli, wanafunzi wanajengewa uwezo wa kuwa viongozi bora na huwashirikisha wakike na kiume bila ubaguzi, lengo ni kutengeneza taifa lenye viongozi bora wa baadae. Mwanafunzi Aisha Khamis Ayoub ambae ni Waziri wa Fedha skuli ya sekondari ya Idrissa Abdulwakil Kizimbani Wete ana...