Skip to main content

Posts

Showing posts with the label SHERIA YA HABARI

TAMWA-ZANZIBAR: 'WAANDISHI PIGIENI DEBE HADI IPATIKANE SHERIA MPYA YA HABARI'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba, wametakiwa kuendelea kutilia mkazo, suala la upatikanaji wa sheria mpya na rafiki ya habari Zanzibar Hayo yameelezwa Disemba 9, 2024 Afisa Program na mchechemuzi wa mpitio za sheria za habari Zanzibar, kutoka TAMWA-Zanzibar Zaina Abdulla Mzee, alipokuwa akifungua mafunzo ya ukumbusho wa sheria hizo, kwa waandishi wa habari wa Pemba, yaliofanyika ofisi ya TAMWA-Pemba. Alieleza kuwa, waandishi wa habari ndio wahusika wakuu wa sheria hiyo, hivyo wanaowajibu wa kupigia debe na kuandika juu ya madhara yaliopo kwenye sheria zilizopo. Alisema, mchakato wa upatikanaji wa sheria mpya, umekuwa ukionekana kwa mwendo wa kusua sua, hivyo waandishi wa habari, wanaweza kutumia kalamu zao, kuchapuza mchakato huo. ‘’Waandishi wa habari, mnaweza kuchapuza kwa haraka mchakato wa upatikanaji wa sheria mpya, kwa kutumia vipindi na makala mbali mbali, zinazoelezea changamoto za sheria zinazitumika sasa,’’alisema. Akiwasilisha vifungu cha sh...