NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ TUME ya Kurekebisha sheria Zanzibar, imesema itaangalia kwa kina, juu ya mifumo ya sheria, ili isiwaweke nje ya utaratibu watu wenye ulemavu, katika mapambano dhidi ya udhalilishaji wa wanawake na watoto. Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu wa Tume hiyo, Mussa Kombo, wakati akikikfungua kikao kazi, cha kupokea maoni ya wadau wa haki jinai, kuelekea marekebisho ya Sheria ya Adhabu nambari nambari 6 ya mwaka 2018 na ile ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai nambari 7 ya mwaka 2018, kilichofanyika ukumbi wa wizara ya Fedha Gombani. Alisema, ni kweli watu wenye ulemavu wanaonekana kuwekwa nyuma kwenye mifumo ya haki jinai, kuanzia kuchukuliwa maelezo vituo vya Polisi, ushahidi mahakamani, kujitetea jambo ambalo, linaweza kuwa chanzo cha kuwakosesha haki zao. Alieleza kuwa, kupitia marekebisho hayo na kwa kuzingatia maoni yaliotolewa, watahakikisha kundi hilo sasa linawekewa kifungu maalum ndani ya sheria hizo, ili iwe sababu ya kuunga mkono mapambano hayo