Salha ZJMMC@@@@ Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mh e . Riziki Pembe Juma amesema S erikali imeamua kuwawezesha wanawake jasiri ili kuwawezesha kiuchumi na kuweza kujitegemea weneyewe ili kuondokana na hali ya utegemezi katika jamii. Ame yasema hayo wakati akifungua mafunzo ya wanawake shupavu wa amali ya Zanzibar yaliyofanyika B weni katika Chuo cha Ufundi Karume Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi , Unguja. Amesema kutoa mafunzo kwa wanawake wenye ujasiri kunaongeza uwezo zaidi wa kuweza kuzalisha bidhaa zao zenye ubora. Pia ametoa wito kwa wataalamu jasiri wanaopatiwa mafunzo ya kuwa walimu kwa wanawake wengine ambao hawajapata fursa ili kuwawezesha wanawake wengi kuweza kujiajiri na kuondokana na utegemezi katika familia zao. Hata hivyo ametoa wito kwa wanawake kuwapenda, kuwaongoza, na kuwalinda watoto wote ili kuwasaidia kuepukana na vitengo vya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji . Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Ra...