Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MIAKA MINNE YA DK MWINYI

MIAKA MINNE YA DK. MWINYI IKULU YA ZANZIBAR WAKULIMA WA MWANI SASA KUHEMEA KIVULI

                                          NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ NOVEMBA 3 ya miaka minne iliyopita, ilikuwa ndio siku ya kwanza ya Rais mpendwa wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuwasili ndani ya Ikuklu ya Zanzibar. Kwa  wakati huo, hakuwasili akitokea nchi jirani..laaahasha alitokea kwenye viwanja alivyokula kiapo, kushika hatamu ya uongozi. Maana Dk. Mwinyi, baada ya kumalizika kwa kampeni za zaina yake, zilizotajwa kama za kisayansi, kwa kule kukutana na makundi mbali mbali, kisha wananchi walimpigia kura. Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa vyama vingi, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC, ilimtangaaza Dk. Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar kwa kupata asilimia 76.27 na kuwaacha mbali wagombea wenzake. ‘’Nimepokea ushindi kwa mikono miwili na nawashukuru wananchi wa Zanzibar, kwa kunichagua mimi na chama changu, kwa miaka mitano ijayo,’’alisema wakati huo. Kwa wananchi Zanzibar, kama alivyosema Mwenyekiti wa CCM mkoa wa kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa, kuwa duniani viongozi