Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amelitaka Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), kuongeza jitihada katika usimamizi na kuhakikisha malengo ya chuo ya muda mrefu na muda mfupi yanafikiwa kama ilivyokusudiwa. Waziri Riziki ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Uongozi wa Chuo hicho iliyofanyika katika Ukumbi wa IAA, Arusha. Amesema Chuo cha Uhasibu Arusha kimeamua kujitofautisha na vyuo vyengine kwa namna mbalimbali ikiwemo kuanzisha mitaala ya kipekee mfano mitaala ya uanagenzi (apprenticeship), kuanzisha mitaala inayoandaa wataalam wanaoweza kujiajiri na kuajiri wengine, kutengeneza miundombinu na mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia. Hivyo ametoa rai kwa Baraza hilo kuhimiza juhudi za kuboresha ubora wa elimu inayotolewa na chuo, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mitaala itakayoanzishwa katika kipindi cha utekelezaji wa majukumu yao ili inaendel...