NA WAANDISHI WETU, PEMBA@@@@ WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi CCM, 270 wakiwemo wanawake 71 na wanaume 199, wamejitokeza kuomba nafasi za Ubunge na Uwakilishi katika majimbo 18 kisiwani Pemba. Kati hao 270, walioomba nafasi ya Ubunge wote walikuwa ni 147, kati ya hao wanawake ni 40 na wanaume 107, huku kwa nafasi ya Uwakilishi wote waliomba ni 123, wakiwemo wanawake 31 na wanaume 92. Waandishi wa shirika la Magazeti ya serikali ambao walifika ofisi za CCM za wilaya za Micheweni, Wete, Mkoani na Chake chake, walibaini kuwa, wilaya ambayo wanawake walijitokeza kwa wingi ni wilaya za Micheweni na Mkoani ziliokuwa na watia nia idadi sawa ya 19 kwa nafasi ya Ubunge na Uwakilishi kila wilaya. Wilaya iliyoshika nafasi ya tatu kwa wanawake wa CCM kujitokeza kwa wingi ni wilaya za Wete, iliyoibua wanawake 17, huku wilaya ya Chake chake ikishika nafasi nne kwa watia nia 16. Aidha wilaya ambayo wanawake waliojitokeza kwa wingi kwa nafasi ya Ubunge ni wil...