HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ AFISA Mkuu wa Mawasiliano na Uchechemuzi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA- Zanzibar Sophia Ngalapi, amesema iwapo habari za kupinga udhalilishaji zitaandikwa na kufanyiwa ufuatiliaji (follow up) zitasaidia kupunguza vitendo hivyo nchini. Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kisiwani Pemba, juu ya mbinu bora za kuandika habari za udhalilishaji, alisema habari hizo zimekuwa zikiandikwa kwa muda mrefu, ingawa imeonekana bado waandishi hawazifanyii ufuatiliaji. Alisema kuwa, hali hiyo imebainika baada ya TAMWA kufanya utafiti kupitia vyombo vya habari, na kugunduwa kuwa zipo habari za udhalilishaji zilizoripotiwa, lakini hazina ufuatiliaji jambo ambalo, linarejesha nyuma juhudi za mapambano hayo. "Utafiti mdogo wa miezi mitatu uliokusanya vyombo vya habari vya redio, magazeti na mitandao ya kijamii, lakini changamoto kubwa iliyoonekana, ni habari za udhalilishaji, kutofanyiwa uf