NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ PAMOJA na kukua kwa uchumi, uimarishaji wa miundombinu ya barabara na ongezeko kubwa la vyombo vya usafiri, imebainika kuwa, kama Jeshi la Polisi na wananchi hawakushirikiana, vifo vitokanavyo na ajali za Piki piki (boda boda) hazitopungua nchini . Imeonywa kuwa, kwa kuliachia jukumu la kupunguza ajali za piki piki Jeshi la Polisi pekee, haitokuwa dawa ya kupunguza ajali hizo, ambazo pia husababisha vifo na vilema. TAKWIMU ZA AJALI ZA PIKI PIKI Uchunguuzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi, umebaini kuwa, kwa mfano kwa mwaka 2019 hadi mwaka 2020 kwa Tanzania, kulikuwa na ajali za piki piki 1,133 zilizosababisha vifo 674 , sawa na majeruhi 948 . Imebainika kuwa, kati ya ajali hizo, Tanzania bara kuliripotiwa ajali 964, zilizosababisha vifo 573 na majeruhi 767 kwa miaka hiyo miwili. Wakati kwa Zanzibar, kuliripotiwa ajali 169 sawa na vifo 101 huku idadi ya majeruhi wakiwa ni 181 . Katika kipindi cha Januari hadi Disemba pekee kwa mwak...