Skip to main content

Posts

Showing posts with the label WATU WENYE ULEMAVU

AFANDE KALFAN: 'KUZIKABILI CHANGAMOTO ZA WATU WENYE ULEMAVU NI JUKUMU LETU'

NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@  JAMII imetakiwa kutoa ushirikiano kwa watu wenye ulemavu kwa kuwasaidia mambo wanayoyahitaji, ili kuweza kushiriki shughuli mbali mbali bila ya usumbufu. Akizungumza na wananchi baada ya kumkabidhi kigari cha kutembelea Hijra Khalfan Hamad mwenye ulemavu wa viungo, Mkaguzi wa shehia ya Pandani Inspekta wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khalfan Ali Ussi alisema, kila mmoja kwa nafasi yake ana wajibu wa kuwasaidia watu wenye ulemavu. Alisema kuwa, watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ambazo husababisha kukosa fursa ya kushiriki kwenye mambo yanayowahusu, jambo ambalo linawanyima furaha katika maisha yao. "Katika kampeni yetu ya nyumba kwa nyumba ya Familia yangu haina uhalifu, tulimkuta mama huyu akatuelezea changamoto yake ya kukosa kigari cha kutembelea, niliona ni muhimu kwake na ndio maana nimekuja leo kumpeleka," alisema Mkaguzi huyo. Alisema kuwa, Jeshi la Polisi limeamua kuweka wakaguzi kwenye shehia ili kusudi kui...