HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ ‘UKIMUELIMISHA mwanamke umeielimisha jamii nzima' Kutokana na msemo huo, inadhihirika kuwa mwanamke ni muhimili mkubwa, katika dunia hasa pale anapoonekana kuwa na nafasi kubwa ya ulezi ndani ya familia. Ingawa haimaanishi kwamba, baba si muhimu hapana nae ana umuhimu wake mkubwa tu, lakini kwa upande wa mama anaechukuwa nafasi ya ulezi wa familia ni jambo kubwa. Na ndio maana, inafahamika kuwa dunia isingeweza kuendelea mbele bila ya uwepo wa wanawake, kwani kuwekeza kwa wanawake na wasichana kunaleta matokeo makubwa. Wanawake wanahitaji kuwa na nyenzo madhubuti zitakazowawezesha kuyamudu maisha yao na kuondokana na utegemezi, ambao unaweza kuwa kikwazo katika kuendeleza mbele maisha yao. Pamoja na kuwepo mafanikio na juhudi za wanawake katika sehemu mbalimbali ikiwemo za kiuchumi, na kijamii bado inaonekana suala la mabadiliko ya tabianchi, linaendelea kuwa na madhara makubwa kwa wanawake. Wanawake wanazidi kuonekana kama watu walio kat...