J oyce Joliga,Tunduru Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Tanzania Dkt. Oswald Masebo alitoa ushauri mzito wa kuyataka Mabaraza ya Mila na Desturi kutumia matamasha ya kumbukizi yatumike kukemea vitendo vya unyanyasaji Watoto, wenye umri wa siku 0 hadi miaka 8 Watoto hao wanekuwa wajikutana na vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji ,ulawiti ambavyo vimekithiri kwenye jamii ili kujenga jamii bora ambayo inaenzi mila na Desturi za kitanzania. Kadhalika ameyataka Mabaraza ya Mila na Desturi kukemea vitendo vya ushoga ambavyo vimekithiri nchini vikiwemo na vitendo viovu vinavyokwenda kinyume na mila na desturi ya mtanzania. Ikumbukwe kuwa Ushauri huu wa D kt.Masebo ametoa ushauri huo kwenye kongamano la kumbukizi ya mashujaa wa vita ya Majimaji lililofanyika kwenye ukumbi wa Crasta mjini Tunduru. Kongamano hilo ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 118 ya mashujaa wa vita ya Majimaji waliuawa na wajerumani Februari 27,1906 kwa kunyongwa mashujaa 67 na