Na Mwandishi wetu OMKR Mwenyekiti wa Nuru Foundation Mama Zainab Kombo Shaib ambae pia ni mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais amesema Jumuiya yao imeamua kujikita zaidi kumuangalia mtoto wa aina yeyote hasa yatima na anaeishi kwenye mazingira magumu Ameeeleza hayo wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea watoto wenye vichwa maji na mgongo wazi katika kituo chao cha nyumba ya matumaini iliyopo eneo la Mwanakwerekwe ndani ya Wilaya ya Magharibi B. Mama Zainab amesema kumlea mtoto mwenye kichwa maji na mgongo wazi kunahitaji elimu kwa mzazi na walezi ili kufahamu namna ya kumlea hatimae nae mtoto akuwe katika mazingira mazuri yaliyo salama katika hali zote Am...