NA HAJI NASSOR, PEMBA::: HATIMAE mahakama maalum ya kupambana na makosa ya udhalilishaji Mkoa wa kusini Pemba, imemswekwa chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka 10, mshitakiwa Khamis Juma Chumu ‘ soda ’ (76) mkaazi wa Mtoni Chake Chake, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 13. Hakimu wa mahakama hiyo Muumini Ali Juma, alisema kati ya adhabu hiyo, mshtakiwa atatumikia chuo cha mafunzo miaka 10 kwa kosa la ubakaji wa mtoto huyo. Akisoma hukumu hiyo, alisema upande wa mashtaka ulifanikiwa kuwasilisha mashahidi watano kwenye kesi hiyo, akiwemo mtoto mwenyewe, ambae alitosha kwa kiwango kikubwa, ushahidi wake kuishawishi mahakama. Alisema, mtoto ndio shahidi mkuu anayepaswa kuihakikishia mahakama kuwa, alibakwa na kutorosha ama laa, na sio mtu mwengine yeyote. Hakimu huyo akiendelea kusoma hukumu hiyo alisema, wakati mtoto huyo wa miaka 13 anatoa ushahidi wake mahakamani hapo, akiongozwa na wakili wa serikali Ali Amour Makame, a...