Skip to main content

Posts

Showing posts from February 9, 2025

ZURA YAWATAKA WAANDISHI KUTOA ELIMU MATUMIZI SAHIHI YA UMEME KWA WANANCHI

NA KHAULAT SULEIMAN, PEMBA@@@@  KAIMU Mkuu kitengo cha uhusiano  Mamlaka ya udhibiti wa huduma ya maji na nishati Zanzibar (ZURA)  Shara Chande Omar amesema mamlaka itaendelea kuandaa utaratibu pindi tu inapotokea mabadiliko ya bei  elekezi kwa matumizi za huduma ya maji,  nishati ili Kuwaondoshea usumbufu wananchi.  Ameyasema hayo  akitoa ufafanuzi wa bei mpya ya umeme katika kikao na  wandishi wa habari mbali mbali huko kwenye ukumbi wa mikutano Ofisi za ZURA Kibirinzi chake chake Pemba Amesema lengo la kikao hicho na wadau wa habari ni  kuwafikishia wananchi tarifa hiyo ya mabadiliko ya bei ya umeme ambayo imeanza kutumika kwa sasa.  " Wandishi wa habari ndio Wenye jukumu la kuwafikishia wananchi tarifa  sahihi pindi tu itapotokea mabadiliko ili kuepuka malalamiko na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya umeme. "alisema kaimu huyo.  Aidha amesema kuwa mamlaka imeanda utaratibu wa kuwasajili mafundi wa umeme kwa kuwapatia vib...

IDARA YA KATIBA: ‘’KUJITOLEA KWA WASAIDIZI WA SHERIA NI TAKWA LA KISHERIA’'

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MKUU wa Divisheni ya Katiba na Sheria Pemba Bakari Omar Ali, amewasisitiza wasaidizi wa sheria, kukumbuka kuwa ,   bado dhana ya kujitolea kwa aina ya kazi yao hiyo, itabakia pale pale licha ya changamoto walizonazo. Alisema, kwa mujibu wa sheria inayowaongoza, ni kosa kutoa elimu, ushauri na msaada wa kisheria na kisha kuomba malipo kwa m wananchi husika. Mkuu huyo wa Divisheni, aliyasema hayo leo Febuari 09, 2025  ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ wakati akitoa maoni yake, baada ya kuwasilisha matokeo ya awali ya utafiti kwa wasaidizi wa sheria ,   kisiwani humo. Alisema, ijapokuwa sasa wapo wanaodai malipo kama baraka ya kufanyakazi zao, lakini bado sheria haitambuwi uwepo wa posho kama motisha wa kufanya kazi zao. Alieleza kuwa, msingi mkuu wakati wa lipo omba kazi hiyo na sasa ikiingizwa ndani ya sheria yao, ni kufanyakazi kwa njia ya kutolea, na hasa kwa wananchi wanyonge na makundi maa...