Ujumbe wa serikali ya Oman ambao upo nchini kwa ziara ya siku 10 leo unakwenda Bagamoyo mkoani Pwani kuangalia eneo la ujenzi wa viwanda, ili uwekezaji huo uanze mara moja. Hatua hiyo ambayo ilielezwa katika taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inaleta matumaini ya kumwagika kwa ajira mbalimbali ndani ya muda mfupi ujao. Akizungumza Ikulu, jijini Dar es Salaam baada ya majadiliano na Rais John Magufuli, taarifa hiyo ilisema, Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dk. Mohammed Hamad Al Rumhy alisema yeye na ujumbe wake wa watu 300 watakwenda Bagamoyo leo kuangalia eneo la ujenzi wa viwanda, ili kazi hiyo ianze mara moja. “Mhe. Rais tunataka kushirikiana nanyi kuendeleza ukanda wa uwekezaji wa Bagamoyo,” taarifa ya Ikulu ilimkariri Dk. Al Rumhy akisema. “Tunataka Bagamoyo isiwe eneo la bandari tu, bali pia liwe ni eneo ambalo tutajenga viwanda mbalimbali, tuzalishe mbolea na tununue mazao ya wakulima na kuyasafirisha. “Sisi tupo tayari na kesho (leo) tunakwenda kuangalia en