HABIBA ZARALI, PEMBA::: LICHA ya serikali kuimarisha huduma za akina mama na watoto mijini na vijijini, ili wajifungulie hospitali, bado jitihada hizo zinaonekana kubezwa na baadhi ya akina mama hao. Tayari Unguja na Pemba serikali imesogeza karibu vituo vya afya na kutowa elimu afya ya uzazi tofauti na zamani, wapo akina mama hujifungulia majumbani wakisaidiwa na wakunga wa jadi. Ni dhahir kuwa akina mama wanapobeza maelekezo hayo na kuamuwa kubakia majumbani hadi kujifunguwa kunaweza kuwaletea madhara yatokanayo na uzazi. Na ndio maana serikali kupitia wizara ya Afya, wakawataka wakunga wa jadi kuwasindikiza mama wajawazito hadi katika vituo vya afya na sio kuwazalisha wakiwa majumbani. Na ndio maana hata Raisi wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi katika hutuba zake za mara kwa mara, huitaka wizara ya Afya kutowa huduma bora na kuona kwamba kunapunguwa vifo vya mama na mtoto. Uchunguzi wa makala h...