NA ZUHURA JUMA, PEMBA SERIKALI ya awamu ya nane inayoongozwa na Dk. Hussen Ali Mwinyi imelichukua suala la uwekezaji wa visiwa vidogo vidogo Zanzibar katika hatua nyengine ambayo ni nzuri na yenye manufaa kwa nchi. Agosti hadi Septemba mwaka 2021, Serikali ilitangaza awamu ya kwanza ya uwekezaji, ambapo visiwa vinane (8) vilipata wawekezaji kati ya kumi (10) vilivyotangazwa. Visiwa hivyo ni Changuu, Pwani, Bawe, Pamunda A na B, Kwale, Chumbe, Misali, Njau na Matumbini A, ambapo kisiwa cha Njau na Matumbini A wawekezaji walishindwa masharti. Serikali imeweka vigezo maalumu kwa wawekezaji wa visiwa na ikiwa hakufikia, hatopatiwa kwani Serikali iko makini kwenye suala hilo. Anasema Mkurugenzi Uwekezaji Pemba Al-haji Mtumwa Jecha, awamu ya pili ilitangazwa mwaka huu, ambapo kwa Pemba ni kisiwa cha Matumbini, Jombe na Kwata Kusini na Kashani, Njau na Fundo Kaskazini. Visiwa hivyo vitakodishwa muda mrefu ili vijengwe hoteli za kitalii zitakazotoa huduma mbali mbali na utakuw