NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANANCHI wa shehia ya Shungi wilaya ya Chake chake Pemba, wamesema kwa muda mrefu sasa, hawana shida tena ya huduma ya maji safi na salama, kufuatia urekebishaji mkubwa uliofanywa na Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA, tawi la Pemba. Walisema kwa sasa wanapata nafasi ya kujipangia muda wao wa shughuli za kilimo, biashara, wajasiriamali na wanaokwenda ofisini, baada ya kuwepo kwa huduma hiyo ya uhakika. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi shehiani hapo, walisema haijawahi kutokea, kwa mud mrefu kuwa na huduma hiyo kwa uhakika, ingawa sasa miaka karibu mitatu hawana wasi wasi. Walisema, kuwa shughuli zao za kujitafutia huduma za chakula na safari nyingine sasa, zimekuwa zikipangika vyema, kwani hapo awali walikuwa wakisuumbuka kutokana na huduma hiyo. Mmoja kati ya wananchi hao Asma Said Abdalla wa Chanjamjawiri, alisema kwa upande wake sasa, amepata utulivu wa kujipangia shughuli zake, kutokana na uwepo wa uhakika wa huduma yam aji safi na sal...