NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imelipongeza Shirika la Magazeti ya serikali, kwa ubunifu wao wa kuanzisha jarida maalum, la kutangaaza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa wananchi. Hayo yameelezwa na Waziri wa hiyo Zanzibar, Tabia Maulid Mwita, wakati akizungumza na masheha wa wilaya nne za Pemba, kwenye hafla ya ugawaji wa jarida hilo, iliyofanyika ukumbi wa Mfuko wa Hifadhi Jamii Zanzibar ‘ZSSF’ Tibirinzi Chake chake. Alisema, uongozi wa Shirika hilo, umezitekeleza kwa vitendo ahadi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, pale alipowataka wakuu wa taasisi kuwa wabunifu, ili kuwafikia wananchi. Alieleza kuwa, ubunifu huo ambao umezalisha jarida la kueleza kwa upana yale yaliyotekelezwa na serikali, utasaidia sasa kwa wananchi kuyaona kwa vitendo. Waziri Tabia alieleza kuwa, ingawa vyombo vya habari vya serikali vipo ikiwemo ZBC, lakini kupitia jarida hilo, kumeongeza wigo kwa wananchi, kuyasoma ya...