Skip to main content

Posts

Showing posts from August 27, 2023

HIVI NDIVYO UISLAMU UNAVYOUKUBALI UZAZI WA MPANGO, IPO NJIA YA ENZI NA ENZELI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KUFUATA uzazi wa mpango, haihusiani na kuzaa watoto kidogo. Uislamu unafafanua kuwa, hakuna uhusiano wowote kati ya kuzaa watoto kidogo, eti chanzo kikawa ni kufuata uzazi wa mpango. Kumbe, kutajwa suala la uzazi wa mpango na Muumba, alishajua ili mtoto aweze kupata virutubisho na mjengo wa mwili, kiakili, mifupa na ngozi, anyonye maziwa ya mama yake. Ndio maana Mhadhiri chuo Kikuu cha Zanzibar ‘SUZA’ Profesa Issa Haji Zidi, anasema uzazi wa mpango, ambao uislamu unaukubali, sio jambo kubwa, bali ni kumuacha mtoto kunyonya miaka miwili. Kufanya hivyo, ndio hujenga huruma, mapenzi, udugu wa kiafya kuanzia ya mama na mtoto mwenye, ijapokuwa pia humpa nafasi baba kujipanga tena. Kumbe, hata mwanamme anapata wasaa wa kucheza cheza na mke wake vyema, iwapo uzazi wao, utakuwa ni wa mpango, kama ambavyo Muumba, ameagiza. ‘’Wapo wanaume hukesha kwenye vibanda vya starehe kwa usiku mkubwa, akikumbuka kwenda kwake na idadi ya watoto wasiopishana, huona