NA HAJI NASSOR, PEMBA MKUU wa mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, amewahakikishia masheha mkoani humo, kuwa watakosa kazi na kisha kusughulikiwa kisheria, ikiwa watasimama kama mashahidi kuzifanyia sulhu kesi za udhalilishaji. Alisema kwa sasa imekuwa ni mchezo endelevu mkoani humo, kwa baadhi ya masheha kujihusisha na sulhu kwa kesi za ukatili na udhalilishaji, jambo ambalo amesema sasa imetosha. Mkuu huyo mkoa aliyaeleza hayo, wakati akilighairisha kongamano la kujadili changamoto za matendo ya ukatili na udhalilishaji, lililofanyika hivi karibuni mjiji Chake chake, lililoandaliwa na Jumuiya ya Tumaini Jipya Pemba TUJIPE. Alisema kama kuna sheha ameshachoka kuhudumu kwenye nafasi hiyo, ajaribu kuzitia mkono kesi hizo, ambazo kwa sasa zimekuwa zikijotokeza siku hadi na kuvizisha juhudi za serikali na wadau wake. Alieleza kuwa, sasa kila sheha lazima ajitenge mbali na kushiriki kwenye jamvi au vikao vya sulhu, baina ya wazazi wa pande mbili, na akigundulika hatua...