NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MRATIBU wa miradi kutoka Mwenvuli wa asasi za kiraia Pemba ‘PACSO’ Mohamed Najim Omar, alisema wanatekeleza kwa vitendo, maono ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha elimu ya uraia na demomkrasia inawafikia wananchi. Mratibu huyo aliyasema hayo, wakati akizungumza na watendaji wa serikali na wanaasasi za kiraia, katika kongamano la pamoja, la kujenga ushirikiano, baina pande mbili hizo, kupitia mradi wa ‘uraia wetu’ lililofanyika Wawi Chake chake. Alisema, mradi huo ni tokeo moja wapo la maono ya viongozi hao, ambapo wameamua kuwakusanya watendaji wa serikali na wale wa asasi za kiraia, ili kuibua changamoto zinazokwamisha ushirikiano wao. Alieleza kuwa, washiriki wa kongamanio hilo, watapata nafasi ya kuelezea changamoto zao kikanuni, sera na kisheria ili kuona zinatatuliwaje kwa umoja wao. ‘’Sote ni mashahidi kuwa, wakati viongozi wetu wanaingia ...