NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANASIASA Kisiwani Pemba, wamesema kazi iliyofanywa na PEGAO, ZAFELA na TAMWA ya kuibua kero za wananchi na kuzifikisha eneo husika, na kisha kuchukuliwa hatua, hakuna mwanasiasa yeyote engeweza kuifanya kazi hiyo. Walisema, taasisi hizo zilifika katika wilaya zote nne za Pemba, na kukutana wananchi, wakiwemo wanawake na kuzisikiliza changamoto zao, na kisha kuzifika tasisi husika kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi. Wakizungumza kwenye mkutano maalum wa kuwasilisha utendaji kazi kwa wahamasishaji jamii hao, kupitia mradi wa kuiwezesha jamii kudai haki zao za uongozi, siasa na demokrasia, na kufanyika ofisi ya KUKHAWA, walisema kazi iliyofanywa ni kubwa. Mwenyekiti wa Chama cha wakulima cha AAFP, taifa Said Soud Said, alisema kazi hiyo anaona kusingekuwa na mwanasiasa yeyote, engeweza kuwafikia wananchi na kuchukua kero kwa lengo la kuzipatia sulhu. Alieleza kuwa, kazi hiyo inafaa kuthaminiwa na kuungwa mkono na serikali kuu, kwa kuziwezesh...