Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MAKALA NAOMBA

NAOMBA: MKULIMA ALIYEJIKITA NA KILIMO MSITU, AELEZEA KILICHOMVUTIA

HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ NI majira ya saa 4:00 asubuhi, nilipofika katika bonde la Kigawani kijiji cha Chwale Wilaya ya Wete Pemba, nikitokea Mkoani.  Katika safari  hiyo niliyochukuwa muda usiopunguwa saa 1:30 kwa usafiri wa umma, nikiwa na lengo la kutaka kujuwa changamoto na maendeleo ya kilimo msitu ambacho kinalimwa shehiani humo.   Ilikuwa ni safari yenye kheri kubwa, kwani kukutana na wakulima  wa kilimo msitu, ambao wameamuwa kujikita na kilimo hicho wakiwa na malengo ya kujikwamua kimaisha. Pamoja na wakulima wengine kuzungumza nao  nilipata hamu na shauku kubwa ya kuzungumza na mkulima Naomba Shaaban Mbarouk, baada ya kumsikia kuwa alikotokea  hakuwa na hamu ya kujiingiza katika kilimo hicho.    Wala sikufanya ajizi nilimvuta pembeni, chini ya muembe huku upepo ukitupepea taratibu akiielezea makala haya, kinaga ubaga kuhusu kilimo hicho kilichomvutia hadi kujiingiza.   Alijiingiza katika kilimo hicho, baada ya kupata mafun...