Skip to main content

Posts

Showing posts with the label BIDHAA BORA

WAJASIRIAMALI WAOMBA KUPATIWA MBINU UZALISHAJI BIDHAA BORA

  NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@ WAJASIRIAMALI kisiwani Pemba wameomba kupatiwa elimu ya usarifu wa bidhaa, ili waweze kutengeneza zenye ubora na viwango, ambazo zitauzika katika   soko la ndani na nje ya Pemba. Wajasiriamali hao walitoa ombi hilo katika mafunzo ya ujuzi wa kidijitali yaliyofanyika kituo cha uwalimu TC Wingwi wilaya ya Micheweni Pemba. Biamu Omar Mbrouk mwanakikundi cha hapa kazi cha Wingwi, kinachojishughulisha na utengenezaji wa sabuni, mafuta na unga wa mwani, alisema wamekua wakitengeneza bidhaa, ingawa zinashindwa kupata soko, kutokana na kukosa ubora. Alisema mwani umebainika kuwa ni moja ya dawa inayotibu magonjwa mengi katika mwili wa mwanadamu, hivyo ni vyema kupatiwa elimu, ili wawe wazalishaji bora. ‘’Tunatamani siku moja kuona kwamba, na sisi tunaziuza Tanzania bara na hadi nchi za nje bidhaa zetu, kwani kutatuwezesha kutambulika na pia kuinua uchumi wetu,’’alisema. Ali Khatib Ali mjasiriamali wa kikundi cha Tumuombe Mola cha Makangale, kina...