Skip to main content

Posts

Showing posts with the label KIDUTANI NA KANUNI

KIDUTANI WAPITISHA KANUNI KUSIMAMIA MALEZI YA VIJANA WAO

    NA MOZA SHAABAN, PEMBA @@@@ KAMATI ya maadili na taaluma ya kijiji cha Kidutani shehia ya Chumbageni Wilaya ya Mkoani Pemba, imepitisha kanuni 19 zitakazowaongoza katika kusimamia malezi ya watoto na vijana. Akizungumza kijijini hapo   katika kikao cha kupitisha kanuni hizo kilichoandaliwa na   kamati hiyo Mwakilishi wa sheha ambae pia ni Mratibu wa kamati ya maadili ya shehia hiyo Abrahman Mohamed Khamis alisema, Ofisi ya sheha ipo tayari kushirikiana na wanakijiji   katika kusimamia kanuni hizo. Alisema ni vyema wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kamati hiyo, ili lengo liweze kufanikiwa, huku akiwataka wanakamati hao iwapo patakua na kikwazo chochote katika utekelezaji majukumu yao, kupeleka changamoto zao kwa sheha. "Ofisi ya sheha ipo tayari kushirikiana na nyinyi katika hili, naomba na wananchi mutoe ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha jambo hili, na iwapo patatokezea kikwazo   katika utendaji kazi wenu musisite kuripoti kwa sheha...