NA HAJI NASSOR, PEMBA:::- MAHAKAMA ya Mkoa Wete, leo Juni 15, mwaka huu inatarajia kupokea mashahidi na kuwasikiliza kwenye shauri la daktari Is-haka Rashid Hadid, wa kituo cha afya Gombani, anayedaiwa kumbaka mara tatu, mtoto wa miaka 16. Shauri hilo linatarajiwa kuendelea leo, baada wiki mbili zilizopita (Juni 1, mwaka huu) kughairishwa, kufuatia upande wa mashataka, kutopokea mashahidi wa kesi hiyo. Awali daktari huyo, alipelekwa rumade kauanzia Mei 18, mwaka huu na kutakiwa kurudi tena mahakamani hapo Juni 1, ili kuwasikiliza mashahidi. Ingawa upande wa mashataka siku hiyo, haukupokea mashahidi, na mtuhumiwa huyo kulazimika kurejeshwa tena rumande, kama sehemu ya kuupa nafasi upande wa mashtaka kuwasilisha mashahidi. Awali, Juni 1, mwaka huu mara baada ya mtuhumiwa huyo kuwasili mahakamani hapo akitokea rumande, chini ya hakimu wa mahakama maalum ya makosa ya udhalilishaji, Mwendesha mashataka Juma Mussa, aliiomba shauri hilo kughgirishwa. Alidai kuwa siku hi...