NA ZUHURA JUMA, PEMBA @@@@ WAANDISHI wa habari kisiwani Pemba wametakiwa kufuata maadili ya kazi zao, ili kuepuka kuingia kwenye makosa. Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari, leo Mei 18, 2024 uliofanyika ukumbi wa Chuo cha Samail Gombani Chake chake Pemba, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud, alisema mwandishi wa habari aliesomea fani ya habari hawezi kuvunja miiko na maadili. Alisema kuwa, tasnia ya habari sasa imevamiwa na watu ambao hawakusomea fani hiyo, jambo ambalo linaweza kusababisha migogoro katika jamii na kushusha hadhi ya tasnia, hivyo ipo haja kwa waandishi wa habari kuzingatia maadili wakati wa kazi zao ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza. "Siku hii ya uhuru wa habari ni muhimu kujitafakari kwamba tunafanya kazi kwa kiasi gani, tuna uhuru kiasi gani, vikwazo gani tunavyopitia na kupanga mikakati ya kuweza kutatua," alisema Mkuu huyo. Mkuu huyo ali...