NA HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@ S HUGHULI za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi , bado zinazidi kuwafanya wananchi na mashirika mbali mbali duniani kujitokeza kwa kutoa elimu ama kugawa mbegu kajili ya kutokomeza j anga hilo. Matumaini makubwa huonekana katika sehemu zenye bahari kwa kuwepo na miti ya mikoko kwa kuepusha athari pembezoni zinazoweza kuepukika . Katika kisiwa cha Zanzibar , kwa sasa kuna uhutaji wa elimu juu ya uwoto wa asili , kwani hupoteza twasira ya mazingira na uharibifu. Matumaini ya wanawake wa kisiwa cha P emba shehia ya M changamdogo ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi , kwa kujikita katika kilimo msitu cha upandaji wa miti ya mikoko. Mikoko ni misitu inayopatikana katika nchi za joto sana na la kiasi , ambayo inaweza kuota na kumea katika maeneo ya maji chumvi , ambayo yapo katika ukanda unaofikiwa na maji kujaa na kutoka na kupwa. Mikoko inaweza kuishi kwa kufunikwa na maji kujaa n...