KATIKA jitihada za kuhakikisha Tanzania inafanikisha utekelezaji wa malengo manne ya kizazi chenye, Jukwaa la Wanawake Wanaelimu wa Afrika, Zanzibar (FAWE Zanzibar) inawezesha wanawake Zanzibar kukabiliana na vikwazo kiuchumi. Kwa kushirikiana na UN Women Tanzania, FAWE Zanzibar inachangia ufikiaji wa malengo hayo kupitia utekelezaji wa Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa wa Kuharakisha Maendeleo ya Kiuchumi kwa Wanawake Vijijini (JPRWEE) unaolenga kuhakikisha ustawi wa wanawake vijijini na haki zao. Utekelezaji wa mpango huo unaenda sambamba na utoaji wa mafunzo kwa wanawake ili kuwasaidia kupata ujuzi wa biashara, elimu ya kifedha, pamoja na fursa za kupata mikopo ili kuanzisha na kukuza biashara zao. Miongoni mwa mafanikio yaliyoelezwa na wanufaika wa mradi huo ambao unatekelezwa Mkoa wa Kusini Unguja ni kuongezeka kwa ajira, hali iliyoboresha kipato cha kaya na kupunguza utegemezi kwa waume. Walisema mradi huo umewawezesha wanawake wengi kuanzisha biashara ndogo n...