Skip to main content

Posts

Showing posts from September 22, 2024

TULIA ACKSON MGENI RASMI LEO HAFLA UTOAJI TUNZO

  NA HAJI NASSOR, DAR-ES-SALAAM@@@@ SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, jioni ya leo Septemba 28, 2024 kwenye hafla ya 15 ya kuwakabidhi tunzo waandishi wa habari mahiri. Tunzo hizo ambazo zimekuwa zikiandaliwa na Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’, kwa mwaka wa 15, tokea zilipoanzisha mwaka 2009, zinatarajiwa kufanyika ukumbi wa AGA KHAN DIAMOND JUBILEE eneo la Upanga jijini Dar-es Salaam. Akitoa taarifa hiyo jana, Katib Mtendaji mpya wa ‘MCT’ Ernest Sungura, alisema matayarisho yote yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa mgeni rasmi huyo. Alisema, Spika huyo ndie atakaemkabidhi mshindi wa jumla kwa mwaka 2023/2024, huku washindi wingine mbali mbali wakikabidhi zawadi na tunzo zao, na wageni mashuhuri waalikwa. Alieleza kuwa, katika hafla inayofanyika jioni hii ya leo, kutakuwa na mambo kadhaa mazuri ikiwa ni pamoja na zawadi kwa mwandishi nguli aliyefanya vyema zaidi katika maisha yake ya kihabari. ...