Skip to main content

Posts

Showing posts from June 14, 2026

MRADI WA ‘PAMOJA’ WABISHA HODI PEMBA, WAANZIA WILAYA YA CHAKECHAKE KWA MAJARIBIO, WANANCHI WAUFURAHIA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ TAKWIMU kutoka Mtakwimu Mkuu wa serikali Zanzibar, zinaendelea kutishia usalama wa wanawake na watoto wa Unguja na Pemba. Maana, kwa miaka mkitatu iliyopita, imekusanya matukio 4,991 ya ukatili na udhalilishaji, ambao wengi wa waathirika ni wanawake na watoto. Ijapokuwa, namba inaonesha kupungua kila mwaka kwa miaka hiyo, lakini kwa juhudi za serikali, washirika wake wa maendeleo, taasisi binafsi na mtu mmoja mmoja, bado maumivu yapo. Maana mwaka 2023, ilikusanya matukio 1,954 ingawa mwaka uliofuata, yalishuka na kuripotiwa matukio1,8 09, na mwaka jana, yakashuka tena na kuripotiwa matukio 1,228. Utaona kuwa, mwaka 2023, matukio 1,954, yalioripotiwa, ingawa mwaka 2024 kulikuwa na mapungufu ya matukio 145, maana yalikuwa 1,809 na mwaka 2025, kukiripotiwa pungufu ya 581 kati ya yale yaliokusanywa 1,228. Hapo sasa, ndio maana kwa Zanzibar nzima, ukiyakusanya matukio hayo kwa kipindi kuanzia mwezi Januari 2023 hadi Disemba 2025, utabaini matukio ...

HAYA HAPA MAGUMU YA UDHALISHAJI WANAYOPITIA WANAWAKE WAJASIRIAMALI

  NA MOZA SHAABAN, PEMBA@@@@ UKATILI na udhalilishaji dhidi ya wanawake na wasichana unasalia kuwa kitendo cha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani kote. Ambapo kila mwaka makadirio ya wanawake milioni 316 sawa na asilimia 11 ya wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 45, hukutana na vitendo hivyo duniani kote, kwa mujibu wa mitandao ya kijamii. Udhalilishaji huo unaweza kua wa kimwili, kingono au kihisia. Takwimu za mwaka 2024 za Shirika la Afya Duniani (WHO), zinaonyesha mwanamke mmoja, kati ya watatu amewahi kufanyiwa ukatili huo katika kipindi cha maisha yake. Kwa mujibu wa takwimu za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar, zilizotolewa na ofisi ya Mtakwimu mkuu wa serikali,   mwaka 2024 kulikuwa na 1,809 ya ukatili na udhalilishaji wameripotiwa. Takwimu hizi zinaonyesha waathirika wengi walikua watoto ambao ni asilimia 84.3 ikifuatiwa na wanawake ambao ni asilimia 11.7. Aidha utafiti uliofanywa na shirika lisilo la kiserikali, linaloendeleza us...