NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ VIJANA 150, waliojiajiri uchimbaji mawe, shehia za Mchakwe, Bwegeza, Kengeja, Shamiani na Mwambe wilaya ya Mkoani, wamesema wamerejesha matumaini ya uhakika wa kipato, baada ya serikali kutengua uwamuzi wake, wa kupiga marufuku uchimbaji wa rasimali hiyo. Walisema, kuanzia juzi Novemba 14 mwaka huu, wameanza kurudi kwenye eneo lao walilojiajiri, kufuatia katazo la awali la serikali, kutengeuliwa mapema wiki iliyopita. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, walisema kwa sasa wanauhakika wa maisha, maana eneo hilo, ndio walilolichagua kiajiri. Walisema, kutenguliwa kwa agizo hilo, kwao ni faraja maana wengi wao, wanazofamilia zinazowategemea, katika maisha yao ya kila siku. Mmoja kati ya vijana hao, Hamad Mcha Vuai wa Mchakwe Mwambe, alisema kwa sasa anajisikia faraja, kutokana na uamuzi huo, wa serikali. ‘’Sasa watoto wangu wataniita baba na mke wangu ataniita muume wangu, maana nimerudi kwenye ajira, nilioichagua, kwa ajili ya kuendeleza...