NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ KITUO cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’, kimewakaribisha wananchi wa shehia za Uwandani wilaya ya Chake chake, kufika ofisini kwao, kwa ajili kupatiwa ufumbuzi wa migogoro mbali mbali ya kisheria, kama vile ya ardhi, tena bila ya malipo. Kauli hiyo imetolewa leo April 13, 2025 na Mwenyekiti wa kituo hicho Pfro: Chris Maina Peter, alipokuwa akizungumza na wananchi hao, kwenye kambi maalum ya siku tatu inayoendelea skuli ya Uwandani. Alisema, kituo hicho hakijasita kutoa ushauri, elimu na msaada wa kisheria bila ya malipo kwa wananchi wasiokuwa na uwezo, kwani sio muda wa kukaa kinyonge kwa wananchi. Profesa Chris, alisema bado mpango wa kituo hicho ni kuendelea kuwasaidia wenye changamoto kama za kukoseshwa vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa na fidia kwa ardhi zao. ‘’Ni kweli leo tupo hapa shehia ya Uwandani kwa muda wa siku tatu, tumewafuata wananchi lengo ni kuwasikiliza ikiwa wanachangamoto za mambo ya kisheria, kuwasaidia bila ya malipo,’’alifa...