Skip to main content

Posts

Showing posts from September 18, 2022

MKOA WA RUVUMA WATOA CHANJO YA POLIO KWA ASILIMIA 122.2

Joyce  Joliga, Songea:::: Songea. Watoto 398,029 sawa na asilimia 122.2.Mkoani Ruvuma wamepatiwa chanjo ya Polio  ili kuwaepusha na ulemavu. Katibu Tawala Msaidizi ,Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii Mkoani Ruvuma Dk.Lous Chomboko amesema Mkoa ulilenga kuchanja Watoto 325,746 katika awamu ya tatu ya kampeni dhidi ya chanjo ya polio iliyoanza Septemba mosi hadi Septemba nne 2022. “Utekelezaji wa kampeni ya utoaji chanjo ya polio ya matone awamu ya tatu kwa Watoto chini ya miaka mitano  umefanyika kwa mafanikio makubwa,mikakati yetu  ni kuongeza wigo wa ufuatiliaji toka ngazi ya Mkoa hadi Halmashauri ili kudhibiti kabisa polio’’,alisisitiza Dk.Chomboko. Amesema serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO lilitangaza uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa polio  Februari 17,2022 katika jiji la Lilongwe nchini Malawi,hivyo Tanzania iliamua kufanya kampeni ya utoaji chanjo dhidi ya polio kwa Watoto chini ya miaka mitano ili kuudhibiti.  Mkoa wa Ruvuma ulikuwa kinar

'TAKRIBANI WATOTO 800 HUGUNDULIKA KUWA NA SARATANI KILA MWAKA'

  Joyce Joliga, Songea::: Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Septemba 23, 2022 ameweka wazi kuwa, kila mwaka takriban watoto 800 hugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani nchini Tanzania hivyo kuchangia ongezeko la vifo vinavyotokana na ugonjwa huo. Waziri Ummy amesema hayo katika kikao  na Taasisi ya Global HOPE iliyoko Texas nchini Marekani katika mkutano wa pembezoni baada ya Mkutano Mkuu wa 77 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea New York, nchini Marekani. "Kila mwaka takriban watoto 800 hugundulika kuwa na ugonjwa wa Saratani nchini Tanzania, lakini kama Serikali tumeendelea kuboresha matibabu ya Saratani kwa watoto ili kuokoa maisha yao." Amesema Waziri. Ummy. Ameendelea kusema kuwa, inakadiriwa kuwa watoto wenye saratani wanaoendelea kuishi zaidi ya miaka miwili kuanzia kugundulika ni kati ya 20% hadi 40%, huku katika nchi zilizoendelea ni zaidi ya 80%, hii ni kutokana na  kuchelewa kufanya uchunguzi, *kuasi* matibabu,  gharama za usafiri na malazi,  uc

WENYE WATOTO WALEMAVU PEMBA WAPEWA MBINU KUWAKINGA NA UDHALILISHAJI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA:::: WAZAZI na walezi wanaoishi na watoto wenye ulemavu kisiwani Pemba, wametakiwa kuzidisha ulinzi zaidi kwa watoto wao, kwani wadhalilishaji wamekuwa wakiwatumia zaidi, kumalizia shida zao za kibinadamu, kutokana na mazingira yao. Ushauri huo umetolewa na Afisa Mipango wilaya ya Chake chake Kassim Ali Omar, wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la watu wenye ulemavu kudhalilishwa, wilayani humo. Alisema, pamoja na shughuli za kila siku walizonazo wazazi na walezi za kutafuta maisha, lazima wajiwekee utaratibu wa kuwawekea ulinzi maalum, watu wenye ulemavu. Alieleza kuwa, haiwezekani wazazi au walezi, wawatelekeze watoto wao majumbani, kwa muda mrefu, bila ya kuwepo mwangalizi maalum. ‘’Shughuli za kutafuta maisha ni nzito, lakini suala la kuwapa ulinzi watu wenye ulemavu, hutakiwa lifanywe mara dufu, maana sasa wadhalilishaji wamehamia kwao, wakijua hawawezi kujitetea mahakamani,’’alieleza. Katika hatua nyin

''MASHAHIDI NJOONI MAHAKAMANI NAULI YENU IPO'

  NA HAJI NASSOR, PEMBA::::: MAHAKAMA kuu kanda ya Pemba, imesema itahakikisha sasa inawapatia stahiki zao zote mashahidi wanaofika mahakamani, ikiwa ni pamoja na nauli, ili kusiwe na mkwamo wa kesi hasa za udhalilishaji unaosababishwa na mashahidi. Hayo yameelezwa leo Septemba 21, 2022 na Naibu Mrajisi mahakamu hiyo kisiwani Pemba Faraji Shomari Juma, wakati akizungumza na waandishi wa habari mahamani Chake chake, pembeni ya kikao kazi za kusukuma kesi, kilichofanyika mahakamani hapo. Alisema, kwa sasa mahakama imeshajipanga vizuri, kuhakikisha mashahidi wanaofika mahakamani, wanapatiwa stahiki zao zote, ikiwemo nauli na kuona hakuna kesi inayokwama, kwa kukosa mashahidi. Alieleza kuwa, kesi kadhaa zikiwemo za udhalilishaji wa wanawake na watoto, zimekuwa zikikwama kutokana na mashahidi kutofika mahakamani, na kusema ikiwa sababu ni kuogopa kukopwa nauli na mahakama, sasa hilo halipo tena. ‘’Ni kweli tumegundua kuwa, kesi nyingi zimekuwa zikifutwa ama kuondolewa mahakamani,

'SHERIA ZINAZOLINDA HAKI ZA WANAWAKE ZITEKELEZWE KWA VITENDO'

                           NA HAJI NASSOR, PEMBA::::: WANAWAKE wa kiislamu ambao wanachuma mali pamoja na waume zao, wametakiwa kufuatilia haki zao za kupatikana kwa mali, mara baada ya ndoa kuvunjika, kwani sheria ya Mahakama ya kadhi, nambari 9 ya mwaka 2017 imetoa haki hiyo. Ilielezwa kwenye sheria hiyo, kifungu cha 5 (1) (f) kuwa, mwanamke aliyeachwa na ikiwa wamechuma mali pamoja na aliyekuwa mume wake, anaweza kulalamika mahakamani, kupata mchango wa kuanzia maisha. Hayo yalibainika hivi karibuni, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ofisi ya PEGAO, Chake chake, wakati Mkurugenzi wa asasi hiyo Hafidh Abdi Said, alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi hao, juu ya utekelezaji wa haki za mwanamke. Alisema, wapo baadhi ya wanaume wamekuwa wakichuma mali pamoja na mwanamke, ingawa baada ya ndoa kuvunjika, hajali na wala hazingatii suala la kumpa mchango wowote mwanamke, kwa ajili ya kuanzia maisha. Alieleza kuwa, ndio maana wakati umefika sasa, kwa wanawake walio

'WAFIKISHENI HOSPITALI HARAKA MNAPOWAGUNDUA NA DALILI HIZI.........'

   NA HAJI NASSSOR, PEMBA:::: JAMII ya Zanzibar, imeshauriwa kuwapeleka hospitali haraka, ndugu na jamaa zao, wanapowaona na dalili kadhaa ikiwa ni pamoja na kutokwa na jasho lisilo la kawaida hata kwa msimu wa baridi, kwani hiyo ni moja ya dalili za kuugua kifua kikuu. Dalili nyingine za kifua kikuu zilizoanishwa ni kikohozi cha wiki mbili zau zaidi, kutoa makohozi yaliyochanganyika na damu, kukonda na kupungua uzito kusiko kwa kawaida pamoia na homa za mfululizo. Hayo yameelezwa na mtaalamu kutoka kitengo shirikishi cha maradhi ya ukoma, kifua kikuu na Ukimwi Zanzibar, Said Khamis Ahmada, wakati akiwasilisha mada ya kifua kikuu, mbele ya waandishi wa habari, kwenye mkutano uliofanyika leo Septemba 18, 2022 , Maabara ya afya ya jamii Wawi Chake chake Pemba. Alisema jamii, haina njia mbadala wanapowagundua wapendwa wao na moja ya kati ya dalili hizo au na nyingine, bali wawafikishe vituo vya afya na hospitalini, ili kufanyiwa uchunguuzi wa afya zao. Alieleza kuwa, maradhi ya